Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Katika hali ambayo zimesalia siku kadhaa tu hadi kufanyika Mkutano wa Berlin-2 kuhusu hali ya mambo ya Libya; wanamgambo wenye mfungamano na Kamanda Haftar wamesema kuwa sasa wanakidhibiti kivuko cha mpakani cha Asin kilichoko baina ya mpaka wa Libya na Algeria.
Kamanda wa kikosi cha 128 cha Kamanda Haftar ameonyesha picha ya wapiganaji wa kikosi hicho wakiwa katika kivuko hicho. Hatua hiyo ya wapiganaji wa Haftar ya kudhibiti kivuko hicho cha mpakani inahesabiwa kuwa hatua ya kwanza kuwahi kushuhudiwa baada ya kufikiwa mapatano ya kusitisha vita huko Libya tarehe 23 Oktoba mwaka jana.
Katika upande mwingine, baada ya wanamgambo wa Haftar kudhibiti kivuko cha Asin, Baraza la Uongozi huko Tripoli mji mkuu wa Libya likiwa ndilo msimamizi wa ngazi ya juu wa jeshi limeagiza kuwa ni marufuku misafara yoyote ya kijeshi kusafirisha silaha na zana za kijeshi bila la kuwasiliana na baraza hilo.
Bunge la Libya hadi sasa limeshindwa kuandaa katiba ya nchi hiyo kutokana na kupambana moto vita vya ndani nchini humo na kushtadi hitilafu za kisaisa kati ya makundi ya nchi hiyo.
342/